Mapema chanzo cha serikali kilichozungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP kwa sharti la kutotambulishwa kilisema hakuna njia au mfumo mwingine wowote wa kuwasiliana na kila sekta itaathirika.

Hii ni mara ya kwanza kuchukuliwa hatua kama hii nchini Afghanistan ambayo itapelekea “kuzimwa kabisa kwa mtandao,” hii ikiwa ni kulingana na shirika la NetBlocks la mtandao na usalama wa mtandao lenye makao yake mjini London.

Kundi la Taliban limeanzisha msururu wa vizuizi vya kupambana na “uvinjifu wa maadili” kama unavyofafanuliwa chini ya sheria kali za Kiislamu tangu liliporejea madarakani mwaka 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *