Jaji wa shirikisho siku ya Jumatatu amezuia mpango wa utawala wa Trump wa kuwafuta kazi mamia ya wafanyakazi katika shirika la utangazaji la Marekani/Sauti ya Amerika (VOA). Katika uamuzi huo mkali, aliwashutumu maafisa kwa dharau na kukiuka utawala wa sheria, linaandika Gazeti la New York Times.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Katika uamuzi ambao shirika la habari la AFP limeona, Jaji wa Shirikisho Royce Lamberth ameamua kwamba kuachishwa kazi, hatu ambayo ingeanza kutekelezwa siku ya Jumanne, Septemba 30, “isitekelezwe” hadi uamuzi wa mwisho utakapotolewa. Jaji huyo aligundua kuwa utawala wa Trump ulishindwa kuzingatia majukumu ya shirika la serikali linalohusika na vyombo vya habari vya umma, USAGM, ambalo linasimamia VOA.

Jaji amesitisha mipango hiyo huku pia akichunguza iwapo shirika husika husika la Marekani, USAGM, shirika la shirikisho linalosimamia vyombo vya habari vya umma vya Marekani, lilitii amri iliyotolewa mwezi Aprili. Makubaliano hayo yalibainisha kuwa shirika hilo lazima litimize dhamira yake ya kisheria ili VOA ifanye kazi kama “chanzo cha habari kinachoaminika na chenye mamlaka.” Kulingana na nyaraka za mahakama, zaidi ya wafanyakazi 500, ikiwa ni pamoja na wengi wa wafanyakazi wanaosalia wa VOA, wameathiriwa na kuachishwa kazi. USAGM na mkurugenzi wa shirika la habari Kari Lake walitangaza kupunguzwa kwa kazi mwishoni mwa mwezi Agosti, kuanzia Jumanne. Aliteuliwa na Rais wa Marekani Donald Trump mwanzoni mwa muhula wake wa pili.

Mnamo mwez Machi, Donald Trump aliishutumu Sauti ya Amerika kwa kutangaza “propaganda dhidi ya Marekani” na upendeleo. Kisha alitia saini agizo la kirais akitaka kituo hicho kifungwe. Hata hivyo, mwishoni mwa mwezi Aprili, utawala wa Trump ulishtumiwa na jaji wa shirikisho. Sauti ya Amerika ilianzishwa wakati wa Vita vya Pili vya Dunia ili kueneza ujumbe wa Marekani katika nchi ambazo uhuru wa vyombo vya habari ulikuwa mdogo au haukuwepo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *