
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa maadui wanafanya kila wawezalo kuiwekea vikwazo Iran kwa sababu nchi hii iimekataa kuwapigia magoti na haitakubali kudhalilishwa.
Rais Pezeshkian amepuuzilia mbai yale yote yanayokususiwa na maadui dhidi ya nchi hii na kuyataja kuwa ni ndoto. “
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana lilirejesha vikwazo kwa Iran vikwazo ambavyo vilikuwa vimeondolewa kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015. Vikwazo hivyo kwa mara nyingine tena vitapelekea kuzuiwa mali za Iran zilizoko nje ya nchi, vitasitisha mikataba ya silaha ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kulenga mpango wake wa ulinzi wa makombora.
Hatua hii imechukuliwa siku mbili baada ya Marekani na waitifaki wake kama ilivyotabiriwa kuipigia kura ya veto rasimu ya azimio lililokuwa limewasilishwa na China na Russia lililotaka kuakhirishwa utekelezaji wa utaratibu wa Snapback ndani ya makubaliano hayo ambao ungepelekea kurejeshwa vikwazo.
Pezeshkian amesema serikali itafanya kila kitu kwa ajili ya heshima ya taifa. Itafanya juhudi kutatua matatizo na kutumia rasilimali zote kwa ajili ya wananchi, ambao wanalengwa na vikwazo vya kiuchumi vilivyorejeshwa dhidi ya nchi hii.
Rais wa Iran wakati huo huo amewakosoa wanasiasa wa Marekani na Ulaya wanaozungumzia haki za binadamu na demokrasia na kusema tazameni yale yanayofanywa na wanasiasa hao huko Gaza. Amesema utawala ambao umeibua hali ya mchafukoge katika eneo haujawahi kuwekewa vikwazo katika Baraza la Usalama kwa sababu Marekani inapinga maamuzi ya nchi nyingine kwa kupiga kura ya veto.