Kulingana na Makamu wa Rais wa Venezuela Delcy Rodriguez jana Jumatatu, amri hiyo inamruhusu Maduro kukusanya vikosi vya jeshi kote nchini humo.

Wiki iliyopita Maduro alisema atawasilisha agizo hilo ili liangaziwe, lakini haijulikani ni lini lilitiwa saini. Mamlaka hiyo itakuwa na uhalali kwa siku 90, ingawa kuna uwezekano wa siku kuongezwa, hii ikiwa ni kulingana na katiba ya nchi.

Hatua hiyo inafikiwa wakati Marekani ikiwa imepeleka manowari za kivita katika eneo la Carribean, ambazo imesema ni sehemu ya vita dhidi ya dawa za kulevya katika eneo hilo, lakini serikali ya Maduro inadai kwamba Marekani inapanga njama ya kumuondoa madarakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *