Watafiti wa kijeshi wa China wamefanya majaribio ya ulipuaji wa nyuklia mtawalia ili kuunda nguvu kubwa zaidi ya uharibifu.

Utafiti mpya wa Kichina unaonyesha namna vichwa vingi vya nyuklia vilivyofanyiwa majaribio vinavyolenga shabaha sawa kwa haraka na kwa wakati mmoja. 

Kwa mujibu wa utafiti huo, wahandisi wa kijeshi wa China wametumia mbinu mpya iitwayo nadharia ya mfanano ili kupunguza nguvu za milipuko mikubwa ya nyuklia kuwa majaribio madogo ya maabara yaliyodhibitiwa kwa uangalifu.

Jaribio hilo ambalo lilifanywa na timu ya watafiti wa kijeshi lilichunguza namna silaha hizo zilizofanyiwa majaribi zinavyoweza  kuchanganya nishati haribifu kuunda nguvu kubwa zaidi ya maangamizi kuliko mlipuko mmoja.

Timu ya utafiti ya kijeshi ambayo iliongozwa na Xu Xiaohui, Profesa Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Uhandisi cha Jeshi la Ukombozi wa Watu huko Nanjing ilieleza katika utafiti wake jinsi vichwa vitatu vinavyolenga shabaha sawa kwa mfuatano wa haraka vinavyoweza kuongeza nguvu za uharibifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *