Familia ya watu wanne wameuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Urusi katika eneo la Sumy kaskazini mwa Ukraine, mkuu wa utawala wa kijeshi wa kikanda, Oleg Grygorov, amesema leo Jumanne, Septemba 30 asubuhi. “Jioni hii, adui amelenga jengo la makazi katika kijiji cha Cherneshchyna, katika mji wa Krasnopillya, na drone ya mashambulizi,” ameandika kwenye Telegram.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Waokoaji wametoa miili ya watu wanne waliouawa chini ya vifusi-wazazi na watoto zao, wenye umri wa miaka 6 na 4,” amesema, kulingana na shirikala habari la AFP.

Usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, shambulio kubwa la mamia ya ndege zisizo na rubani na makombora ya Urusi dhidi ya Ukraine lilisababisha vifo vya watu wanne mjini Kyiv, akiwemo msichana wa umri wa miaka 12, na wengine kadhaa kujeruhiwa kote nchini. Urusi ilianzisha mashambulizi katika eneo la Sumy baada ya kukamilisha operesheni yake ya kijeshi mnamo mwezi Aprili kutoka eneo la Urusi la Kursk, sehemu ndogo ambayo ilikuwa imekalia tangu majira ya joto ya 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *