
Kwa wiki kadhaa, hali ya sintofahamu imetawala juu ya mustakabali wa mkataba huu wa kibiashara ulioanzishwa chini ya utawala wa Bill Clinton kati ya nchi 32 za Afrika na Marekani. Muda wake umeisha rasmi leo Jumatano asubuhi saa 12:00 asubuhi saa za Afrika ya Kati, wakati Republican na Democrats walikuwa wakijadiliana kufikia makubaliano ya bajeti ya muda.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hata hivyo, Ikulu ya White House ilikuwa imeonyesha kuunga mkono kusasishwa kwake kwa mwaka mmoja au miwili. Nchi kadhaa za Kiafrika bado zinategemea usaidizi wake.
Mnamo mwaka wa 2023, mauzo ya nje ya Afrika yaliyosimamiwa na AGOA yalikadiriwa kuwa na thamani ya takriban dola bilioni 10. Kulingana na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (UNCTAD), hali hii inapaswa kushinikiza mataifa ya Afrika kufikiria upya ushirikiano wao wa kiuchumi.
Moja ya mifano maarufu ni Lesotho. Nguo zake hazitozwi ushuru wa forodha chini ya mkataba wa AGOA. Leo, inajikuta ikishindana na uagizaji kutoka Vietnam na Ufilipino, ambayo sasa inakabiliwa na ushuru wa chini.
“Hii ina maana kwamba bidhaa zinazouzwa nje na wanufaika wa AGOA zinaweza kujikuta katika hali duni zaidi wakati wa kujaribu kupata soko la Marekani. Nchi zitalazimika kutathmini faida zao za ushindani na kubaini iwapo zinaweza kuendelea kushiriki katika soko la Marekani, kutokana na ushuru ambao bidhaa zao zitakabiliana nazo,” anafafanua Luz Maria de la Mora, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha UNCTAD.
UNCTAD inasisitiza fursa za Kusini-Kusini
Kwa kuzingatia hali ya kutokuwa na uhakika inayotokana na sera ya biashara ya Donald Trump, UNCTAD inahimiza nchi za Afrika kutafuta masoko mapya. “Kwa hiyo ni muhimu kwa wanufaika wa AGOA kubadilisha washirika wao wa kibiashara kwa kushirikiana kimkakati na Umoja wa Ulaya, China, Mataifa ya Ghuba, na mataifa mengine yenye uchumi unaoibukia ili kuhakikisha upatikanaji wa masoko yenye uwiano na kutabirika. Hii ni fursa ambayo lazima tuione kuwa nzuri,” anaoeza Luz Maria de la Mora.
UNCTAD inasisitiza fursa za Kusini-Kusini. Mwaka jana, soko hili lilikuwa na thamani ya dola trilioni 6. Pia inahimiza bara hilo kupanua biashara ndani ya Eneo Huria la Biashara la Afrika.