
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Jumanne, Septemba 30, limeidhinisha azimio lenye lengo la kubadilisha Misheni ya Usaidizi wa Polisi ya Haiti inayoongozwa na Kenya kuwa kikosi imara zaidi, kwa lengo la kujaribu kukomesha vurugu za magenge ambayo yanaendelea kuangamiza Haiti.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakati majukumu ya Ujumbe wa Polisi wa Kimataifa unaoongozwa na Kenya (MMAS) nchini Haiti ukikamilika, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, Septemba 30, lilipiga kura ya kuunga mkono azimio linalolenga kuligeuza kuwa kikosi chenye nguvu zaidi cha kupambana na magenge.
Kwa kura kumi na mbili za kuunga mkono na tatu kutoshiriki, chombo hicho kilipiga kura ya kuunga mkono kuundwa kwake kwa lengo la kukomesha ghasia zinazoendelea kuikumba Haiti. Miongoni mwa nchi zilizojizuia ni pamoja na Urusi na China, ambazo mwaka jana zilipinga mabadiliko ya asili ya MMAS. Moscow na Beijing wakati huu zilielezea shaka juu ya kusuluhisha hali hiyo kwa nguvu na kusisitiza haja ya kushughulikia sababu kuu zilizoitumbukiza Haiti katika machafuko.
Ingawa hakuna upeo sahihi wala ufadhili wa kikosi hiki kipya—ambacho hakitachukua muundo wa misheni ya kulinda amani—bado hakijajulikana, kinapaswa kuwa na rasilimali na wafanyakazi zaidi ili kupambana kwa ufanisi zaidi na magenge yanayodhibiti 90% ya Port-au-Prince, mji mkuu wa Haiti, na wamepanua uwezo wao kwenye majimbo mengine mawili ya nchi. Kwa hivyo nguvu zake zingeweza kufikia hadi askari 5,500—maafisa wa polisi pamoja na wanajeshi—jambo ambalo halikuwa hivyo ndani ya MMAS, ambayo haikuweza kufikisha idadi ya askari 2,500 ambao walipaswa kujiunga na safu zake.
“Mamlaka ya kushambulia”
Tofauti nyingine kubwa: kikosi hiki kipya cha kupambana na genge kitakuwa na “mamlaka ya kushambilia zaidi na hakitaunga mkono tu vikosi vya usalama vya Haiti: pia kitaweza kufanya shughuli zake, ambayo itaipa nafasi zaidi ya kufanya mashambulizi,” anaelezea Diego Da Rin, mtaalam katika shirika la kimataifa la kutatua migogoro (ICG) na mtaalamu wa Haiti, ambaye pia anasisitiza kuwa ufadhili wake utaonekana zaidi. Ingawa itasalia kutegemea michango ya hiari kutoka kwa mataifa, tofauti na MMAS, itatoka “kwa kiasi kikubwa kutokana na michango ya lazima kwa hazina ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani,” anaendelea.
“Kupitishwa kwa azimio hili kunatoa matumaini kwa Haiti. Matumaini ambayo yalififia haraka wakati magenge ya kigaidi yalipopanua eneo lao, ubakaji, uporaji, mauaji na kuwatia hofu wakazi wa Haiti.” “Kupanuka huku kwa vurugu za magenge kumehatarisha uwepo wa taifa la Haiti, kwani shughuli zao zinatishia kubadilisha nchi hiyo kuwa ya wahalifu, ghasia na dawa za kulevya,” amesema Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Mike Waltz.
Tahadhari moja ndogo, hata hivyo, ni kwamba kikosi hiki kipya cha kupambana na magenge hakitarajiwi kutumwa nchini Haiti kwa muda wa miezi sita, kulingana na ICG. Walakini, mamlaka ya sasa ya MMAS inamalizika rasmi siku ya Alhamisi, Oktoba 2…