NAIROBI – Afrika Mashariki inashuhudia mabadiliko kwenye matumizi ya huduma za mitandao baada ya kampuni ya kutoa huduma za mitandao ya Mawingu kupokea ufadhili wa hadi dola milioni 20 ili kupanua wigo wake wa kutoka nchini Kenya hadi Tanzania. Ufadhili huo umetolewa na kampuni ya Pembani Remgro Infrastructure Fund  (PRIF II).

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mjibu wa Farouk Ramji, afisa mkuu mtendaji wa Mawingu, hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa hakuna pengo katika matumizi ya mitandao na pia kuhakikisha huduma za mitandao zinawafikia watu wanaoishi maeneo ya vijijini nchini Tanzania na Kenya.

Maeneo mengi ya vijijini kwenye mataifa ya Afrika Mashariki yamesalia nyuma katika kupata huduma bora za mitandao, jambo linalochangiwa na masuala kama vile ukosefu wa miundombinu, gharama kubwa za ujenzi na changamoto za kijiografia. Hata hivyo, takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa hali ya upatikanaji wa intaneti katika kanda hii inazidi kubadilika.

Uwekezaji huu wa Mawingu utasaidia kukabiliana na changamoto kama vile gharama kubwa za ujenzi wa miundombinu vijijini, upungufu wa nguvu za umeme na kutoelewa teknolojia.

Kwa upande mwingine, mafanikio yatakapopatikana yatakuwa makubwa—kufungua milango ya elimu mtandaoni, ushauri wa biashara na mfumo wa kiuchumi wa kijamii katika jamii ambazo kwa muda mrefu zimekuwa nyuma.

Takwimu na Muktadha wa Kanda

Kanda ya Afrika Mashariki iko miongoni mwa maeneo ya dunia yenye kiwango kidogo cha upatikanaji wa huduma za mitandao. Licha ya hayo, mataifa ya Kenya na Tanzania yanaongoza kwa upatikanaji wa huduma hizo katika kanda ya Afrika Mashariki, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la EACO (eaco.int).

Ripoti ya Benki ya Maendeleo ya Afrika pia imeashiria kuwa benki hiyo imefanikiwa kuunganisha raia wa Afrika milioni 66.5 kutumia huduma za mitandao, hasa katika muongo mmoja uliopita, hatua iliyolenga kupunguza tofauti iliyopo kati ya watumiaji wa mitandao barani Afrika.

Katika karne hii, licha ya changamoto za matumizi ya mitandao, kila raia wa Afrika ana haki ya kuunganishwa na mitandao ili kufahamu kinachoendelea duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *