MECHI ya Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) iliyochezwa leo Oktoba 1, 2025 kati ya JKU na  KVZ kwenye Uwanja wa Mao A mjini Unguja, imemalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Ramadhan Kiparamoto aliitanguliza KVZ akifunga bao dakika ya 18, kisha Feisal Hilali akaisawazisha JKU dakika ya 33 baada ya kupiga kichwa na mpira kujaa kambani.

Erigy Josephy aliongeza la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 37 ambapo bao hilo ilifanya JKU kwenda mapumziko ikiongoza kwa mabao 2-1.

Dakika 45 za kipindi cha pili zilikuwa za moto kwa pande zote mbili, hususani KVZ kusaka bao la pili ambalo lilipatikana dakika ya 56 likifungwa na Majid Bakar.

JKU ilipata bao la tatu lakini lilikataliwa na mwamuzi ikidaiwa kuwa mfungaji aliotea kwani mchezaji aliingia ndani ya boksi.

Katika mechi nyingine iliyopigwa Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba, Malindi dhidi ya Junguni zimeshindwa kufungana.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili, timu ya Mafunzo itaikaribisha New Stone iliyopanda daraja msimu huu kwenye Uwanja wa Mao A na Kipanga dhidi ya Fufuni kwenye Uwanja wa Mao B.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *