Mitaa kadhaa jijini Arusha ilishuhudiwa kuwa na maandalizi ya aina yake ya kumpokea mgombea Urais kupitia chama tawala CCM, ambacho kimekuwa madarakani kwa miaka 48 sasa.

Mgombea urais kupitia chama hicho ambaye pia ndio Rais wa sasa wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amehutubia katika maeneo mbali mbali ya majimbo ya uchaguziya mkoa wa Arusha, akiwanadi wagomea udiwani, Ubunge pamoja na nafasi yake ya kuogombea Urais.

Samia aahidi kujenga masoko na vituo vya mabasi

Katika maeneo mengi aliyopita, mgombea huyo wa CCM ameonekana kuwa na hoja zinazofanana akitaja mafanikio ya uongozi wa chama hicho tangu kimeshika Dola na kuahidi kwamba kazi kubwa zaidi itafanyika tena endapo atachaguliwakatika uchaguzi wa mwaka huu Oktoba 29.

Kwa kutumia kauli mbiu ya “Kazi na Utu” ameahidi kujenga masoko, na vituo vya mabasi.

Mitandao inaweza kushawishi kura yako?

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Lakini pia akiwa katika mkutano wa kampeni  katika jimbo la Arumeru Mashariki, Rais Samia ametoa agizo kwa mabalozi ya nyumba kumi wa chama hicho kuhakikisha kila balozi anatembea katika nyumba zake 10 na kuwachukua watu mpaka vituo vya kupigia kura.

Wananchi wanasema kampeni za mwaka huu hazina ushindani mkubwa kwa CCM, zinaonesha taswira ya kutokuwa na upinzani kutoka kwa vyama inavyoshindana navyo. Lakini nimewauliza baadhi yao, matumaini yao ni yapi katika mchakato huu wote wa uchaguzi?

Rais Samia aliingia madarakani mwaka mwezi Machi mwaka 2021,baada ya kifo cha ghafla cha aliyekuwa Rais wa nchi hiyo John Pombe Magufuli, na anaweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwania kiti cha urais kupitia chama hicho. Veronica Natalis DW, Arusha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *