Wiki ya hotuba, mikutano ya ngazi ya juu, na heka heka za foleni katika mitaa ya Manhattan jijini New York yalipo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa yalihitimishwa rasmi asubuhi ya Septemba 29, na kutuachia takwimu zifuatazo muhimu.

Annalena Baerbock (kushoto), Rais wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akifungua mkutano kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

UN Photo/Loey Felipe

Annalena Baerbock (kushoto), Rais wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akifungua mkutano kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

KIKAO CHA MJADALA MKUU: 80

Mwaka huu 2025 Umoja wa Mataifa unaadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwake. Annalena Baerbock anaongoza kikao hiki, kilichoanza Septemba na atahudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja, chini ya mada: “Bora Pamoja: Miaka 80 na Zaidi kwa Amani, Maendeleo, na Haki za Kibinadamu.”

WASHIRIKI: 12,296

Wakati wa Wiki ya Ngazi ya Juu, hotuba rasmi hutolewa katika Ukumbi wa Baraza Kuu, pembezoni hufanyika mamia ya mikutano mingine inayohusisha wajumbe na viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.

WAZUNGUMZAJI KATIKA MJADALA MKUU: 194

Jumla hii inajumuisha wawakilishi 189 wa Nchi Wanachama, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, na Rais wa Baraza Kuu (hotuba za ufunguzi na za kufunga zimehesabiwa mara moja). Pia inajumuisha waangalizi watatu wa kudumu—Palestina, Holy See, na Muungano wa Ulaya—ambao wamealikwa kuzungumza pamoja na Nchi 193 Wanachama wa Umoja wa Mataifa.

WASIOKUWEPO: 4

Afghanistan, El Salvador, Myanmar, na Ushelisheli.

Afghanistan na Myanmar hazikuhudhuria kutokana na mizozo kuhusu uwakilishi rasmi wa serikali zao.

Ushelisheli haikuwepo kwa sababu ya kuingiliana kwa ratiba ya UNGA na uchaguzi wake wa kitaifa wa urais.

“Sijaenda kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati huu; nilihisi haina maana mwaka huu,” Rais wa Salvador Nayib Bukele aliandika kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa X, pia aliweka video ya hotuba yake ya mwaka jana 2024.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas alirekodi ujumbe wake kupitia video baada ya kunyimwa visa yakuingia Marekani kuhudhuria UNGA jijini New York.

Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu.

UN Photo/Loey Felipe

Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu.

MZINGUMZAJI WA KWANZA: Brazil

Brazili kihistoria imekuwa Nchi Mwanachama wa kwanza kuzungumza katika Mjadala Mkuu (bila kujali kiwango cha uwakilishi) tangu kikao cha 10 mwaka wa 1955, isipokuwa mwaka wa 1983 na 1984.

Mwaka huu, Rais Luiz Inacio Lula da Silva alitoa hotuba ya Brazil.

MZUNGUMZAJI WA MWISHO: Timor-Leste

Balozi Dionisio Da Costa Babo Soares wa Timor-Leste akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa themanini wa Baraza Kuu.

UN Photo/Loey Felipe

Balozi Dionisio Da Costa Babo Soares wa Timor-Leste akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa themanini wa Baraza Kuu.

Dionísio da Costa Babo Soares, Mwakilishi wa Kudumu wa Timor-Leste, katika UN alitoa hotuba ya mwisho ya mjadala wa mwaka huu Jumatatu asubuhi ( tarehe 29 Septemba 2025).

VYEO VYA WALIOZUNGUMZA

Wakuu wa Nchi: 83

Makamu wa Rais: 6

Mfalme: 1

Wakuu wa Serikali: 41

Naibu Mawaziri Wakuu: 4

Mawaziri: 45

Naibu Waziri: 1

Wawakilishi wa nchi wanachama katika Umoja wa Mataifa: 8

Waziri Mkuu Mia Amor Mottle wa Barbados akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha themanini cha Baraza Kuu.

UN Photo/Loey Felipe

Waziri Mkuu Mia Amor Mottle wa Barbados akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha themanini cha Baraza Kuu.

JINSIA: 168 Wanaume, 24 Wanawake

Ushiriki wa wanawake bado ni mdogo lakini unakua (mwaka 2024, viongozi wanawake 19 walizungumza, 5 tu kati yao walikuwa wakuu wa nchi).

Wakuu wa Nchi 8: Dominica, Visiwa vya Marshall, Namibia, Macedonia Kaskazini, Peru, Slovenia, Suriname, Uswisi

2 Makamu wa Rais: Sudan Kusini, Uganda

3 Wanawake Wakuu wa Serikali: Italia, Barbados, Trinidad na Tobago

1 Naibu Waziri Mkuu: Liechtenstein

Mawaziri 8: Austria, Ecuador, Sweden, Iceland, Romania, Ufilipino, Falme za Kiarabu, Canada

Wakuu 2 wa Ujumbe: Denmark, Malawi

Katika hotuba zao wajumbe kadhaa walionesha kumuunga mkono mwanamke kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Chile hata ilitangaza kuwa Rais wa zamani Michelle Bachelet ni mgombea.

Donald Trump (kwenye skrini), Rais wa Marekani, akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha themanini cha Baraza Kuu.

UN Photo/Manuel Elías

Donald Trump (kwenye skrini), Rais wa Marekani, akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha themanini cha Baraza Kuu.

HOTUBA NDEFU ZAIDI: Marekani

Rais Donald Trump wa Marekani alizungumza kwa dakika 57 na sekunde 16.

Alikosoa washirika wa Umoja wa Mataifa na Ulaya, akielezea sera zao za uhamiaji na nishati kama uharibifu, na kutetea mtazamo wa upande mmoja wa “Amerika Kwanza”. Aliangazia mafanikio katika biashara, usalama, na utatuzi wa migogoro, alidai kuwa umepunguza tishio la nyuklia la Iran, na akapendekeza mpango wa alama 21 kwa Gaza chini ya uratibu na Israeli.

Ingawa sheria rasmi katika UNGA inaweka kikomo cha dakika 15 kwa kila mzungumzaji, kiutendaji hotuba nyingi huchukua muda mrefu, na kiti cha Rais wa Baraza Kuu kwa ujumla hubadilika kutokana na muenendo wa wazungumzaji.

HOTUBA FUPI ZAIDI: Ubelgiji

Waziri Mkuu wa Ubelgiji alizungumza kwa dakika 6 na sekunde 44. Bart De Wever alikiri mapungufu ya Umoja wa Mataifa lakini akaeleza kuunga mkono ajenda ya mageuzi ya UN80, akiangazia uwekezaji unaokua wa ulinzi wa Ubelgiji, ushirikiano wa karibu wa Ulaya, na juhudi za kupambana na uhalifu wa kimataifa kupitia ushirikiano wa kimataifa.

MIKUTANO YA KATIBU MKUU: 148

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alifanya mikutano 148 ya mashirikiano na viongozi wa dunia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov alimtania Guterres kuhusu kutokuwepo kwa bendera ya Urusi kwenye picha yao. Guterres alieleza kuwa itifaki ya Umoja wa Mataifa inahifadhi bendera za kitaifa kwa wakuu wa nchi, si mawaziri wa mambo ya nje.

Katibu Mkuu akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi

UN Photo/Eskinder Debebe

Katibu Mkuu akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi

HOTUBA ZA KATIBU MKUU: 20

Guterres alitoa hotuba 20 katika wiki hiyo, ikiwa ni pamoja na maadhimisho ya miaka 80, ufunguzi wa GA, na katika mikutano ya ngazi za juu ya akili mnemba AI na mabadiliko ya mabadiliko ya Tabianchi

VYOMBO VYA HABARI: 3,300

Ofisi ya mawasiliano ya Umoja wa Mataifa ilitoa zaidi ya hati 3,300 kwa waandishi wa habari kutoka karibu nchi 150.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *