Tetemeko kubwa la ardhi lilitokea katikati mwa Ufilipino jana Jumanne usiku limeua watu zaidi ya 70 na kujeruhi wengine kadhaa, maafisa wa eneo hilo wamesema hayo leo Jumatano.

Timu za uokoaji zinaendelea kuwatafuta manusura walionasa chini ya vifusi huku mamlaka husika ikifanya hima kurejesha umeme na usambazaji wa maji uliotatizwa na tetemeko hilo.

Tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa 6.9 kwa kipimo cha rishta lilipiga eneo la kaskazini la Cebu karibu na mji wa pwani wa Bogo, wenye takriban watu 90,000, na kufuatiwa na mitetemeko minne midogo yenye ukubwa wa 5.0 au zaidi.

Waokoaji, askari, maafisa wa polisi, na watu waliojitolea wakiwa na vijiti na mbwa wa kunusa, wanaendelea kuchakura vifusi na mabaki kwa ajili ya kuwasaka walionusurika na kuopoa maiti.

Mamlaka za eneo hilo zimetangaza ‘hali ya janga’ katika maeneo ya Cebu baada ya tetemeko hilo kuangusha majengo, kukata umeme, na kuvunja madaraja.

Gavana wa Cebu, Pamela Baricuatro, ambaye mkoa wake una watu milioni 3.4 na ni kitovu kikuu cha watalii, amesema kiwango kamili cha uharibifu katika Bogo na miji inayozunguka eneo la kaskazini hakijabainika vizuri.

Ufilipino, iliyoko kwenye eneo la Pasifiki ni miongoni mwa nchi zinazokumbwa sana na majanga duniani, yakiwemo matetemeko ya ardhi, maporomoko ya udongo, vimbunga na miripuko ya volkeno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *