Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran amesema kuwa, Marekani haina nia ya dhati ya kufanya mazungumzo.

Dakta Ali Larijani akieleza kuwa nchi za Magharibi zinataka kuishinikiza Iran amesema: “Wakati upande wa Marekani unaposema kwa uwazi kwamba masafa ya makombora yako inapaswa kuwa chini ya kilomita 500, inaonesha kuwa haitaki kuwepo mazungumzo ya kweli.”

Ali Larijani, amesema katika kipindi cha televisheni cha “Katika Ahadi Moja” akizungumzia shakhsia ya Shahidi Nasrullah: “Kuzungumza juu yake kunahitaji muda mwingi, kwa sababu alikuwa mtu mkubwa mwenye sura tofauti, na kushughulikia tu baadhi ya sifa zake haitoshi kumtambulisha.”

Huku akieleza kuwa msururu wa sifa za kimaadili na kiakili zilimfanya awe na shakhsia ya kuvutia na yenye taathira, ameongeza kuwa: “Moja ya sifa zake muhimu ilikuwa fikra zake thabiti kuhusiana na maendeleo ya eneo, hususan nchini Lebanon na ulimwengu wa Kiislamu. Tofauti na baadhi ya watu waliotawanyika katika masuala mbalimbali, yeye daima alikuwa na muono wa wazi wa matukio.”

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran amebainisha kuwa, “mtazamo huu wa kuangalia mustakabali ulimwezesha kuongoza vizuri harakati za kiraia. Ikiwa viongozi hawana maono hayo, kwa kawaida wanatoshheka tu na radiamali za muda na za kimbinu; lakini Sayyid Nasrullah akiwa na maarifa ya hali ya ju na moyo wa kushaurika alifuata njia sahihi katika kukabiliana na matukio.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *