
Watu karibu 40 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa, baada ya kuangukiwa na fito na mbao za kushikilia jengo la Kanisa nchini Ethiopia.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tukio hili limetokea saa moja na dakika 45 asubuhi, siku ya Jumatano kwenye mji wa Arerti, umbali wa Kilomita 70 kutoka jiji kuu Addis Ababa.
Ripoti zinasema, watu hao waliangukiwa na mbao na fito hizo wakiwa kwenye jengo hilo la kuabudu, wakiadhimisha sikukuu ya Bikira Maria.
Picha zilizochapishwa kwenye ukurasa wa facebook wa Shirika la taifa la Utangazaji, limewaonesha watu waliojeruhiwa, huku ikiripotiwa kuwa waliojeruhiwa vibaya, wamepelekwa jijini Addis Ababa kwa ajili ya kupata matibabu maalum.
Ajali kama hizi hutokea sana katika taifa hilo kwa sababu wajenzi walio wengi, hawazungatii tararatibu za ujenzi kwa kuhakikisha kuwa hatua zote za usalama zimeheshimiwa.