
Ripoti ya uchunguzi ya New York Times imefichua undumakuwili na kinga ya wanajeshi wa Marekani wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa kivita nchini Afghanistan, ikihusisha kesi kama vile mauaji ya raia, utesaji na shambulio la hospitali ya Madaktari Wasio na Mipaka na kutofunguliwa mashtaka na kupewa adhabu kali kwa wahusika.
Ripoti hiyo inaangazia kesi mbili mashuhuri: Kesi ya Matthew Golsteyn, afisa wa Kikosi Maalum ambaye alikiri kumuua mshukiwa na kuchoma mwili wake na akafunguliwa mashtaka, katika mkoa wa Kunduz, ambapo, licha ya ushahidi wa kina wa mauaji na mateso ya wafungwa tisa wa Afghanistan, hakuna mjumbe wa Marekani aliyeshtakiwa na kesi hiyo ikafungwa.
Ripoti hiyo imegundua kuwa Kamandi Maalum ya Operesheni ya Marekani iliamua kunyamaza, kuficha, na hata kuwapandisha cheo washtakiwa. Miongoni mwa visa hivi ni shambulizi la anga la 2015 katika hospitali ya Madaktari Wasio na Mipaka huko Kunduz na kuua raia 42 na, licha ya ahadi za uwajibikaji, lakini hakuna afisa mwandamizi aliyeadhibiwa.
Wakosoaji wanasema undumakuwili huu unaakisi utamaduni wa uaminifu wa kibubusa na kinga ya kimuundo ndani ya vikosi maalum vya Marekani. Ufichuaji huo umeibua maswali mazito kuhusu uwazi wa vikosi hivyo, uwajibikaji na kuheshimu sheria za vita.
Hapo awali, wanamgambo wa Taliban wanaotawala nchini Afghanistan walikuwa wamezitaka nchi zilizofanya uhalifu wa kivita nchini humo kulipa fidia na kuwafikisha wahusika wa jinai hizo mbele ya mkono wa sheria.