
Mamia ya wanaharakati, akiwemo Greta Thunberg, mwanaharakati maarufu wa mazingira kutoka nchini Sweden, wamezuiwa na maafisa wa usalama wa Israeli, baada ya kukamatwa kwa meli na boti zilizokuwa zinasafirisha misaada ya kibinadamu kwenye ukanda wa Gaza, huku mataifa kama Qatar yakishinikiza kuachiwa kwao.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wizara ya Mambo ya nje ya Israel, imethibitisha kukamatwa kwa meli na boti hizo kutoka shirika la kimataifa la Flotilla, na wote waliokuwa wanasafiri na misaada hiyo, wamesafirishwa bandarini ili kurejeshwa Ulaya.
Ripoti zinasema, meli hiyo ilizuiwa baada ya kukiuka sheria na kuvuka mpaka wa majini bila idhini, kutoka kwa jeshi la Israeli ambalo linadhibiti mpaka huo, lakini haimiliki eneo hilo la bahari.
Aidha, Israel imessema, ilimtahadharisha nahodha wa meli hiyo kubadilisha njia, wakati ilipokaribia katika eneo linaloaminiwa kuwa la kivita, lakini ikakaidi agizo hilo.
Kipindi hiki cha vita, Israeli imeweka utaratibu, ambao meli au boti zinapaswa kufikia umballi wa maili 70 kutoka pwani ya Gaza.
Wakati hayo yakijiri, Wizara ya afya kwenye ukanda wa Gaza, umesema, watu zaidi ya 70 wameuawa na wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa, kwa saa 24 zilizopita kwa sababu ya mashambulio ya jeshi la Israel yanayoendelea kuwasaka wanamgambo wa Hamas.