
Msafara wa meli, ujulikanao kama Global Sumud Flotilla (GSF), unaobeba misaada kuelekea ukanda wa Gaza ilutangaza mapema leo Alhamisi, Oktoba 2, kwamba unaendelea na safari yake kuelekea eneo lenye vita la Palestina licha ya kuzuiliwa kwa boti zake kadhaa na jeshi la wanamaji la Israel siku ya Jumatano jioni.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
GSF imeshutumu “shambulio haramu dhidi ya wafanyakazi wa kibinadamu wasio na silaha” na kutoa wito kwa “serikali, viongozi wa dunia, na taasisi za kimataifa kudai usalama na kuachiliwa kwa wale wote walio ndani ya boti hizo.”
Israel imekamata “meli kadhaa,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel iesema, ikiripoti boti kumi na tatu zilizobeba jumla ya watu 200. Miongoni mwa abiria waliokuwa kwenye boti zilizozuiliwa ni mwanaharakati wa Uswidi Greta Thunberg, ambaye mamlaka ya Israel imeonyesha kuokota vitu vya kibinafsi, akiwa amezungukwa na watu wenye silaha.
Gazeti la Global Sumud Flotilla (kwa Kiarabu lenye maana ya “ustahimilivu”) limeripoti kwenye mtandao wa kijamii wa X saa 00:20 siku ya Alhamisi kwamba “boti 30 zinaendelea na safari kuelekea Gaza, na ziko umbali wa maili 46 (kilomita 85) licha ya mashambulizi ya mara kwa mara” kutoka kwa jeshi la wanamaji la Israel. “Wamedhamiria kufika Gaza. Wana motisha na wanafanya kila wawezalo kuvunja kizuizi mapema leo asubuhi,” amesema msemaji wa GSF, Saif Abukeshek.
Hatua ya vikosi vya Israel kuzuia msafara huo ni “uhalifu wa uharamia na ugaidi wa baharini dhidi ya raia,” kundi la Hamas, linalotawala Gaza, lilitangaza siku ya Jumatano jioni.
Leo, misaada ya kibinadamu kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kimataifa imezuiwa na haiingii Gaza. Ikiwa misaada ya kibinadamu itawasilishwa kwa Israel, haitaingia Gaza kamwe. Lengo la GSF ni kufikisha misaada hii ya kibinadamu kwa mashirika ya Gaza.