
Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran Hossein Simaee amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Iran Tamaki Tsukada kabla ya kufanya ziara huko Japan kwa lengo la kushiriki katika kikao cha 22 cha Kongamano la Sayansi na Teknolojia katika Jamii (STS).
Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknoljia wa Iran ameyataja mazungumzo kati yake na Balozi wa Japan nchini Iran kuwa ni mwanzo wa ushirikiano mkubwa zaidi kati ya pande mbili katika siku zijazo.
Hossein Simaee amesema anatumai kuwa Iran na Japan zitanufaika na ushirikiano kati yazo ili kuendeleza sekta ya sayansi na teknojia kwa sababu kwa mujibu wa mapendekezo ya UNESCO, vikwazo havijumuishi nyanja ya sayansi na teknolojia; sekta ya sayansi na utafiti haipaswi kuwekewa vikwazo.
Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran ameongeza kuwa: Wairani wana mtazamo chanya kuhusu Japan; na hata katika suala la utamaduni, mshikamano na ukaribu wetu na Japan umekuwa mkubwa kuliko hapo awali. “Tunawafahamu waandishi wengi wa Kijapani, wanafikra wa Kiislamu, na wasomi wa Quran; na mmoja wa watu mashuhuri ambao watu wa Iran wanamfahamu vyema ni Izutsu ambaye alifariki katika miaka ya 1990 na ana nafasi maalumu miongoni mwa Wairani,” amesema Hossein Simaee.
Katika mazungumzo hayo, naye Balozi wa Japan nchini Iran amesema:” Licha ya vizuizi mbalimbali vilivyopo, uga wa sayansi na teknolojia unachukuliwa kuwa jukwaa linalofaa kwa ajili ya kudumisha na kuimarisha uhusiano wa pande mbili kati ya Iran na Japan.”