
Wanaharakati hao waliokuwa katika msafara wa meli takriban 45 wa kupeleka msaada katika Ukanda wa Gaza, walikamatwa na jeshi la Israel katika eneo la bahari ya Kimataifa.
Mandla Mandela na wanaharakati wengine watano wa Afrika Kusini walikuwepo katika msafara huo unaojulikana kama Global Sumud Flotilla (GSF), uliokuwa na nia ya kuvunja uzio wa Israel katika eneo hilo la wapalestina, ili kufikisha misaada Gaza ambako Umoja wa Mataifa umesema tayari eneo hilo linakabiliwa na baa kubwa la njaa.
Jeshi la Israel lilianza kuzizuwia meli hizo jana Jumatano baada ya kutoa onyo kwamba zinakaribia eneo la bahari lililo chini ya udhibiti wake.
Kwa upande wake rais wa Uturuki Tayyip Erdogan amekosoa hatua ya Israel akisema nchi hiyo inaonyesha wazi kwamba haina nia ya kweli ya kuacha matumaini ya amani kushamiri Gaza