Jeshi la wanamaji la Israel limekamata meli zilizokuwa zimebeba misaada kuelekea Gaza na kuwaweka kizuizini wanaharakati waliokuwa ndani, akiwemo mwanaharakati wa hali ya hewa wa Sweden Greta Thunberg.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Msafara huo, ujulikanao kama Global Sumud Flotilla (GSF), ulikuwa na takriban meli 45 zilizobeba wanasiasa na wanaharakati, na uliondoka Uhispania mwezi uliopita kwa lengo la kuvunja mzingiro wa kijeshi wa Israel katika Ukanda wa Gaza – eneo ambalo Umoja wa Mataifa umetahadharisha kwamba linakabiliwa na njaa kali.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel imethibitisha kuwa meli kadhaa za GSF zimezuiwa na abiria wake kuhamishwa hadi bandari ya Israel. Serikali ya Tel Aviv ambayo imelitaja jaribio la GSF la kusafirisha misaada kwenda Gaza kuwa ni “uchokozi” imesema “Greta Thunberg na marafiki zake wako salama na wenye afya.”

Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel  imeongeza kuwa jeshi la wanamaji liliambia meli hizo kubadili mkondo kwa kuwa “zinakaribia eneo la mapigano”.

GSF ilielezea uvamizi huo kama “kinyume cha sheria” na “si kitendo cha kujilinda” bali ni “kitendo cha unyanyasaji “.

Kwa upande wake, GSF imeeleza kuwa hatua ya kuzuiwa kwao ni kinyume cha sheria za kimataifa, na wala sio kitendo cha kujilinda kama inavyodai Israel, bali ni “kitendo cha kukata tamaa kwa dhahiri.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *