Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, ametoa rai kwa wananchi kutojihusisha na vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya umma licha ya changamoto za usafiri zinazojitokeza, akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na hatua kali zitachukuliwa kwa watakaobainika.

Amesema kuwa hali kwa sasa imetulia na kuongeza kuwa mabasi 20 mapya tayari yameanza kutoa huduma katika barabara husika tangu asubuhi, hatua ambayo imepunguza usumbufu na kurahisisha huduma za usafiri kwa wananchi.

#AzamTVUpdates
✍Juliana James
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *