Katika taarifa yake iliyotolewa mjini New York na msemaji wake Guterres amesema shambulio hilo limetokea wakati wa Yom Kippur, siku takatifu zaidi katika kalenda ya Kiyahudi, ambapo mshambuliaji aligonga waumini kwa gari kabla ya kuanza kuwashtukiza kwa kisu.

Kwa mujibu wa duru za habari mshambuliaji huyo aliuawa papo hapo na polisi waliokuwa wakifanya doria, huku polisi wakikamata watu wawili zaidi wanaoshukiwa kuhusika na tukio hilo.

Nyumba za ibada hazipaswi kushambuliwa

Katika taarifa hiyo Katibu Mkuu amesema kuwa nyumba za ibada ni sehemu takatifu ambapo watu wanapaswa kupata amani.

Almeongeza kuwa kulenga sinagogi wakati wa Yom Kippur ni tendo la kikatili. Aliwapa pole waathirika na familia zao, na kuwatakia majeruhi ahuweni ya haraka. Aidha, amesisitiza mshikamano na jamii ya Kiyahudi na kuwataka wahusika kufikishwa mbele ya sheria.

Kuongezeka kwa chuki dhidi ya Wayahudi

Katibu Mkuu pia ameeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu kuongezeka kwa chuki dhidi ya Wayahudi duniani kote na kusisitiza umuhimu wa kukabiliana na chuki na hali ya kutovumiliana katika aina zote.

Amesema “Jamii ya kimataifa lazima ishikamane kuhakikisha matukio kama haya yanakabiliwa kwa nguvu na wahalifu wanakabiliwa na mkono wa sheria”.

Hatua za usalama na uchunguzi

Polisi mjini Manchester imesema inachunguza tukio hili kama shambulio la kigaidi na imeongeza ulinzi katika masinagogi yote nchini Uingereza.

Maafisa wa usalama pia wanachunguza iwapo mshambuliaji alikuwa na vifaa vya mlipuko, huku wakitumia kikosi cha kutengeneza mabomu kuhakikisha usalama wa eneo hilo.

Umoja wa Mataifa unasisitiza umuhimu wa mshikamano wa kimataifa katika kukabiliana na ugaidi na kuhamasisha amani na uvumilivu miongoni mwa jamii zote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *