Kufuatia malalamiko ya wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuhusu huduma zisizoridhisha za mabasi ya mwendokasi, Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza mabadiliko katika uongozi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka (UDART). Hatua hii inalenga kuboresha usimamizi na kutoa huduma bora kwa abiria.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka iliyotolewa leo Oktoba 2, 2025, Rais Samia amemteua Said Tunda kuwa Mtendaji Mkuu wa DART, akichukua nafasi ya Dkt. Athumani Kihamia. Vilevile, Pius Ng’ingo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa UDART, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Waziri Kindamba.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi