
Kando na Maandamano hayo kusitishwa mjini humo miji mingine bado ilishuhudia vuguvugu la vijana wa Gen Z kufika barabarani kudai mageuzi nchini humo.
Wakipata muako wa maandamano ya vijana yaliyofanyika nchini Kenya na Nepal, maandamano hayo makubwa ambayo hayajawahi kuonekana kwa miaka mingi Madagascar yametoa changamoto kubwa kwa serikali ya rais Andry Rajoelina aliyechaguliwa tena mwaka 2023.
Umoja wa Mataifa umesema watu 22 waliuwawa na zaidi ya 100 walijeruhiwa katika maandamano ya wiki nzima. Serikali imesema idadi hiyo sio ya kweli.
Vijana waandamana kupinga mgao wa mara kwa mara wa umeme ambao unakatika kwa zaidi ya saa 12.