Mfalme Charles amesema yeye na mkewe Camilla wamesikitishwa na kisa hicho kilichotokea siku muhimu kwa jamii ya kiyahudi wanapoadhimisha siku kuu ya Yom Kippur.

Mwanamume anayeaminika kutekeleza kisa hicho alilivurumisha gari nje ya sinagogi hilona kuwagonga watu waliokuwa karibu huku kukiwa pia na shambulizi la kisu. Polisi mjini humo imesema imempiga risasi na kumuua mshukiwa huyo ambae hakutajwa jina.

Akizungumza baada ya kukatiza ziara yake Copenhagen kunakofanyika mkutano wa viongozi wa Ulaya juu ya Ukraine, Waziri Mkuu wa UingerezaKier Starmer amesema polisi wamepelekwa katika masinagogi yote nchini humo kuimarisha usalama zaidi kwa mayahudi.  

“Shambulio la Manchester ni la kushtua kabisa na tuko pamoja na waathirika. Niko njiani kuelekea London na nikifika nitakuwa na mkutano wa dharura. Tayari naweza kusema kuwa polisi wa ziada wamepelekwa katika masinagogi yote nchini Uingereza, na tutafanya kila tuwezalo kuilinda jamii ya kiyahudi.”

Starmer amewashukuru maafisa wa polisi kwa namna walivyolishughulikia kwa haraka tukio hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *