Maandamano yanaendelea nchini Morocco, kushinikiza mageuzi kuhusu namna huduma zinavyotolewa kwa wananchi, lakini pia kumaliza visa vya ufisadi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa siku ya sita, siku ya Alhamisi, maandamano hayo yanayoongozwa na vijana maarufu kama Gen Z, yanaendelea kwenye miji mbalimbali ikiwemo Casablanca.

Vijana hao wameunda vuguvugu na kuliipa jina GenZ 212, kupanga maandamano ya amani kulalamikia changamoto mbalimbali zinazotokea kwenye taifa hilo la Afrika Kaskazini, likiwemo pia mageuzi kwenye sekta ya afya na elimu lakini pia kusitishw ubaguzi dhidi vijana na wanawake.

Siku ya Jumatano mauaji ya Kwanza, yalishuhudiwa, baada ya waandamaji kupigwa risasi na kuuawa, kwa madai ya kushambulia kituo cha polisi katika mji wa Agadir.

Tangu kuanza kwa maandamano hayo, karibu wiki moja sasa, wizara ya usalama inasema, imewakamata vijana zaidi ya 400, na wanazuiwa  kwenye vituo mbalimbali vya polisi, baada ya makabiliano makali na maafisa wa usalama

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *