Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameungana na viongozi na waumini wa Kiislam katika dua ya kumrehemu hayati Ali Hassan Mwinyi.
Dua hiyo iliyofanyika katika eneo alilozikwa Rais huyo wa zamani wa Zanzibar na Tanzania, Mangapwani mkoa wa Kaskazini Unguja imeongozwa na ofisi ya Mufti wa Zanzibar na kuhudhuriwa na waumini mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali na CCM kutoka ndani na nje ya Zanzibar.
#AzamTVUpdates
Mwandishi Mtumwa Saidi
Mhariri | @moseskwindi