Bunge la Shirikisho la Somalia jana lilipasisha Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto baada ya wabunge kukutana mjini Mogadishu.

Kikao hicho kiliongozwa na Spika wa Bunge la Wawakilishi katika  bunge la shirikisho la Somalia Sheikh Adan Mohamed Noor Madobe na kuhudhuriwa na wabunge 145.

Taarifa kutoka ofisi ya Spika wa Bunge imeeleza kuwa wabunge 130 walipiga kura kuunga mkono Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto, 10 walipiga kura za hapana, na wabunge 5 walijizuia kupiga kura.

Hatua ya Bunge la Shirikisho la Somalia ya kupasisha mkataba huo ni hatua muhimu katika kuendeleza ulinzi wa kisheria kwa watoto katika eneo lote la Pembe ya Afrika.

Somalia ni nchi ya 52 barani Afrika kuidhinisha mkataba wa haki za binadamu wa kikanda. Morocco, Sudan Kusini na Tunisia ni wanachama pekee wa Umoja wa Afrika ambazo haziridhia mkataba huo hadi sasa. 

Kwa mujibu wa Mkataba huo uliopitishwa awali na Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), ambao baadaye ulibadilishwa jina na Umoja wa Afrika   nchi wanachama zina jukumu la kuzingatia na kukuza haki za watoto, ikiwa ni pamoja na kuwalinda dhidi ya unyanyasaji na kuhakikisha wanapata elimu na huduma za afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *