Umoja wa Mataifa unataka hatua za haraka kuchukuliwa, kuzuia mauaji makubwa ya kikabila yanayoendelea kutekelezwa kwenye mji wa El-Fasher, Magharibi mwa nchi ya Sudan.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wito huu umekuja, baada ya Ofisi ya Tume ya Haki za binadamu, katika ripoti yake kueleza kuwa mashambulio yakiongozwa na wanamgambo wa RSF yameongezeka katika eneo hilo, na kuzua wasiwasi wa mashambulio makubwa Kaskazini mwa Darfur, katika siku za hivi karibuni.

Taarifa ya Volker Turk Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu, imesema mauaji makubwa yanayoendelea pamoja na mateso, yanapaswa kukoma.

Kati ya tarehe 19 hadi 29 mwezi Septemba, Tume hiyo ya Haki za binadamu, imesema, watu 91 waliuwa baada ya kushambuliwa na wanamgambo wa RSF, kwa kile kinachoonekana ni kuwaondoa wakaazi wa El Fasher.

Umoja wa Mataifa, unataka raia wa kawaida kulindwa kwenye mji huo, hasa wale wasiokuwa na uwezo kuondoka El-Fasher, na kuwataka wanamgambo wa RSF na jeshi la Sudan, kukubali misaada ya kibinadamu kuwafikia wenye uhitaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *