Wananchi wameeleza maoni yao baada ya mabasi mapya ya mwendokasi ya kampuni ya MOFAT kuanza kutoa huduma kwa abiria wanaosafiri kati ya Mbezi na Kimara, hatua iliyolenga kupunguza kero ya upungufu na ubovu wa mabasi yaliyokuwepo.

Mabasi hayo yalianza kazi rasmi asubuhi ya leo, saa chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kutangaza utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, lililotaka baadhi ya mabasi ya MOFAT yaliyokuwa yahudumu njia ya Mbagala, yaanze kutoa huduma barabara ya Morogoro ili kupunguza changamoto zilizokuwepo.

#AzamTVUpdates
✍Alpha Jenipher
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *