
Watafiti watano kutoka Taasisi ya Royan nchini Iran wametajwa miongoni mwa asilimia 2 ya wanasayansi wanaonukuliwa zaidi duniani, kwa mujibu wa orodha iliyochapishwa na Chuo Kikuu cha Stanford.
Orodha hii ya kila mwaka, inayotolewa na Stanford, ni ya heshima kubwa katika nyanja za kisayansi, ikilenga kutambua watafiti wenye ushawishi mkubwa katika fani mbalimbali za kitaaluma.
Watafiti hao mashuhuri kutoka Taasisi ya Royan kwa mwaka 2025 ni: Hossein Baharvand, Mohammad Hossein Nasr-Esfahani, Mohammad Reza Baghban Eslaminejad,Reza Omani Samani, Hamed Daemi.
Wote watano ni wataalamu waliobobea katika fani za Tiba ya Kliniki na Biokemia & Baiolojia ya Molekuli.
Kwa mujibu wa orodha ya Stanford, Nasr-Esfahani ndiye mtafiti mwenye uzoefu mkubwa zaidi katika Taasisi ya Royan, akiwa na miaka 36 ya kuchapisha tafiti za kisayansi.
Taasisi ya Royan ni kituo mashuhuri kinachojitolea kwa ushirikiano wa kitaaluma na kitabibu katika nyanja mbalimbali, kwa lengo la kuelewa matatizo ya uzazi kwa wanaume na wanawake, ukuaji wa kiinitete, baiolojia ya seli shina, na teknolojia ya kibaiolojia.
Taasisi hii hutoa huduma kamili za matibabu ya utasa, tiba ya kurejesha seli, uzalishaji wa protini za kijenetiki, na uundaji wa bidhaa za kibaiolojia.