Mlipuko mpya wa Ebola umekuwa ukiendelea tangu mapema mwezi Septemba nchiniJamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika Mkoa wa Kasai. Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), watu 42 wamefariki kati ya wagonjwa 64 waliothibitishwa. Ingawa hatari ya kuenea inachukuliwa kuwa kubwa katika ngazi ya kitaifa, inabakia wastani kwa nchi jirani. Kukabiliana na kuibuka tena huku, kampeni ya chanjo inaendelea na mpango wa kukabiliana umewekwa ili kupunguza kuenea kwa maamukizi ya virusi vya Ebola.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mlipuko wa Ebola uliotangazwa mapema mwezi Septemba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umesababisha vifo vya watu 42 kati ya kesi 64 zilizothibitishwa, lakini hatari ya kuenea kikanda bado ni ya wastani, WHO imesema siku ya Jumatano. Virusi vya Ebola mara nyingi husalia kuwa vibaya licha ya chanjo na matibabu ya hivi karibuni.

Ugojwa wa Ebola umeua watu 15,000 katika bara la Afrika katika kipindi cha miaka 50 iliyopita. Ugonjwa wa Ebola, ambao ni mbaya zaidi nchini DRC, ulitokea kati ya mwaka 2018 na 2020, na kusababisha karibu vifo 2,300 na maabukizi 3,500.

Kampeni ya chanjo ilizinduliwa katikati ya mwezi Septemba nchini DRC, kufuatia tangazo la kuzuka upya kwa ugonjwa wa Ebola katika jimbo la kati la Kasai.

WHO imewasilisha mpango kazi wa kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi.

Katika hatua hii, kesi 64 za Ebola zimerekodiwa nchini DRC, ambapo “42 wamefariki,” mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, katika ujumbe uliotumwa siku ya Jumatano kwenye mtandao wa X. WHO iliwasilisha mpango wa kukabiliana na ugonjwa huosiku ya  Jumatano, Oktoba 1, unaolenga kudhibiti janga hilo katika mkoa wa Kasai.

Kulingana na WHO, mlipuko huo unaosanbaishwa na vifaa vya kinga visivyotosheleza, “ufuatiliaji usio kamili wa mawasiliano, ugunduzi wa marehemu, na desturi zisizo salama za maziko.” “Uhamaji mkubwa wa idadi ya watu” na “utegemezi kwa waganga wa jadi” “unaweka mzigo kwenye mfumo wa afya ambao tayari ni dhaifu na kuongeza hatari ya kuenea kwa ugonjwa huo,” shirika linaongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *