
Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema: “Njia ya kukabiliana na uvamizi na jinai za Wazayuni ni muqawama na kusimama kidete; njia hii imeonyesha kuwa njia pekee ya kuepusha dhulma ni kusimama kidete na kukabiliana na adui.”
Ayatulllah Sayyid Ahmad Khatami amesema hay oleo katika hadhara ya waumini waliohudhuuria ibada ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran ambapo sambamba na kusisitiza udharura wa kuumtaja na kumkumbuuka Mwenyezi Mungu aliwaasa wauumini kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu na kutahadharisha juu ya kupuuza hilo.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesisitiza kuwa, taifa la Iran katu halitakubali kudhalilishwa.
Amesema, hakuna mtu au taifa lenye haki ya kuiambia Iran kwamba, isirutuubishe madini ya urani.
Akikosoa misimamo ya kiudhalili kuhusiana na uwezo wa kiulinzi wa nchi, Ayatullah Khatami amesema: “Baadhi ya watu leo wanasema kuwa Iran isiwe na urutuubishaji madini ya urani, na hapo awali wamesema tusiwe na makombora ya masafa marefu na ya masafa ya kati, ili shambulio likitokea tusiweze kukabiliana nalo na nchi itaangamizwa. Hatukubali mtazamo huu wa kidhalili.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran aliendelea kusema: Wapumbavu hawa hawajui kwamba ikiwa watathubutu kutushambulia, tutaiangamiza Tel Aviv kwanza, na ikiwa wanataka kutuangamiza, raia wa taifa hili wataendelea kwenye njia ya muqawama waliyoichagua.
Ayatullah Khatami ameashiria wimbi la malalamiko ya kimataifa dhidi ya utawala wa Kizayuni na kusema: “Kilio hiki cha kimataifa ni jambo lenye baraka na linapaswa kuungwa mkono. Walimwengu wanapaswa kuonyesha radiamali dhidi ya ukandamizaji wa wavamizi.”