#HABAI: Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuendelea kupeleka pembejeo za mbolea ya ruzuku kwa wakulima wa Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara, ili kuongeza uzalishaji wa mazao, hususani ngano, na kufanikisha azma ya taifa kujitegemea katika chakula hicho muhimu.

Dkt.Samia amesema serikali itahakikisha wakulima wanawezeshwa kuzalisha kwa wingi kupitia ruzuku hiyo, akibainisha lengo la taifa ni kufikia uzalishaji wa tani milioni moja za ngano ifikapo mwaka 2030.

“Niwaahidi kuwa tutaendelea kuwaletea pembejeo za mbolea ya ruzuku, ili tuweze kuzalisha zaidi, lengo letu kitaifa ni kufikisha tani milioni moja ifikapo mwaka 2030, zitoke huku Hanang ili tuweze kujitegemea kwa mahitaji ya ngano, haipendezi kwamba tuna mashamba ambayo yangeweza kuzalisha ngano kwa wingi, lakini tunaagiza ngano nyingi kutoka nje, na huku mashamba yamekaa, hayazalishi”

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *