#HABARI: Issa Ramadhani (35), mkazi wa Mtaa wa Mnyakongo, Kata ya Nkuhungu, jijini Dodoma, anatuhumiwa kubaka na kuwalawiti watoto watatu wenye umri chini ya miaka mitatu, na kuwasababishia majeraha makubwa sehemu za siri.

Mtuhumiwa anadaiwa kufanya matukio hayo kati ya Agosti 12, majira ya saa tano asubuhi, wakati watoto hao walipokuwa wakicheza jirani na makazi yao, akawalaghai kwa kuwaambia wafuate pagala lililokuwa karibu, akidai lina makopo ya kuchezea, ndipo akawafanyia ukatili huo.

Wazazi wa watoto hao walikwenda Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma kuripoti tukio, ambako walipatiwa fomu ya matibabu (PF3) na watoto kupelekwa hospitali kwa huduma za haraka. Matokeo ya vipimo vya kitabibu vilithibitisha kuwa watoto walilawitiwa na kupata majeraha makubwa. Hata baada ya mtuhumiwa kukamatwa, wazazi wamesema wameshuhudia ucheleweshaji wa mchakato wa kisheria.

Mmoja wa watoto amesimulia kuwa walipojaribu kupiga kelele, mtuhumiwa aliwatishia kuwa atawaachia mbwa wawashambulie. Baada ya ukatili huo, alitoroka eneo la tukio.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mnyakongo, Bw. Stephano Chiwaligo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mtuhumiwa ni mtu mwenye akili timamu, ila ni mtumiaji wa vilevi ikiwemo pombe, sigara na bangi.

Aidha Bw. Chiwaligo amesema ofisi yake inafuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi hiyo na ameahidi kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa katika vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka huku akiwasihi wazazi na walezi kuwa makini zaidi katika kuwalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji vinavyoweza kujitokeza.

Video kamili Inapatikana YouTube ##itvtanzania
Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *