#HABARI: Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC) kimesaini makubaliano ya ushirikiano na Taasisi ya Kuimarisha Uwajibikaji nchini (WAJIBU), kwa lengo la kufanya utafiti utakaobainisha changamoto na kutoa suluhisho la muitikio mdogo wa miradi ya ubia nchini.

Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa makubaliano hayo mjini Morogoro, Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila, alisema Tanzania haiwezi kufikia malengo ya kujenga uchumi wa zaidi ya dola trilioni moja kama yalivyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo, iwapo itategemea kodi na mikopo pekee bila kuimarisha maeneo mengine ya ubia na uwekezaji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wajibu, Ludovick Utouh, ambaye pia ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mstaafu (CAG), alisema utafiti huo unatarajiwa kutoa mwanga juu ya sababu kuu za changamoto za ubia na hatua madhubuti za kuchukua ili kuvutia wawekezaji zaidi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *