#HABARI: Mgombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU) Majalio Kyara, ameahidi kumaliza changamoto ya upatikanaji wa soko la uhakika la zao la Tumbaku kwa wakulima kwa kupanga bei elekezi itakayowadhibiti walanguzi kuwanyonya wakulima kwa kuvuna na kuuza kiholela.

Mhe.Majalio alikuwa akiitangaza ilani ya chama hicho na kunadi sera kwa wananchi akiomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo akiwa katika Viwanja vya Mnada Urambo akielekea wilayani Kaliua mkoani Tabora amesema wakulima wengi wanauza Tumbaku lakini hawafahamu malipo yao.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *