#HABARI: Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema ikiwa atapewa ridhaa ya kuongoza katika awamu ijayo atahakikisha kiwanja cha ndege cha Wasso kitafanyiwa ukarabati ili kuruhusu ndege kutua kwa urahisi.
Katika mkutano wake wa kampeni wilayani Karatu mkoani Arusha leo Oktoba 3, 2025, pia mgombea huyo amesema atahakikisha uboreshaji wa barabara zinazoufikia uwanja huo wa ndege na Uwanja wa Ndege wa Ziwa Manyara ili kuwafanya wasafiri kwenda kwa urahisi.
”Tumepokea maombi hapa kutoka Ngorongoro, wamesema kile kiwanja cha Ndege cha Wasso, kifanyiwe ukarabati na ndege ziweze kutua kule. Mipango hiyo tunayo ndani ya Serikali, tunafanya mazungumzo na wenzetu ambao ndio wanakitumia sana kuwanja kile, ili tukifanyie ukarabati, tutanue ile njia na ndege ziweze kutua vizuri,” ameeleza mgombea huyo.
Karatu ni kituo cha mwisho katika zoezi la kampeni mkoani Arusha, ambapo ameelekea katika Mkoa wa Manyara kwa ajili ya kuendelea na kampeni.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.