#HABARI: Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi uboreshaji wa barabara katika wilaya za Karatu na Monduli, mkoani Arusha, ikiwa ni sehemu ya vipaumbele vya CCM katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025/30.

Akizungumza leo Ijumaa, Oktoba 3, 2025, katika mkutano wa kampeni wilayani Karatu, Dkt. Samia amesema Serikali itajenga kwa tabaka gumu barabara yenye urefu wa kilomita 88 kutoka geti la Ngorongoro kuelekea Serengeti, kazi itakayogawanywa katika awamu tatu.

Aidha, amesema ombi la kujenga barabara ya kilomita 10 inayoelekea kwenye hoteli za kitalii litafanyiwa kazi, sambamba na uwekaji wa taa za barabarani kuanzia Mto wa Mbu, Karatu, hadi mpakani mwa geti la Ngorongoro.

Kwa upande wa Monduli, Dkt. Samia amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya Mto wa Mbu–Engaruka yenye urefu wa kilomita 50 kwa kiwango cha lami, na kuongeza kuwa kazi ya uboreshaji wa barabara nyingine katika wilaya hizo itaendelezwa kadri ilani inavyotekelezwa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *