#HABARI: Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, amefikishwa katika mahakama ya Harare, akikabiliwa na shtaka la kupatikana na dawa za kulevya.
Robert Mugabe Jr (33) alikamatwa Jumatano asubuhi alipokuwa akiendesha gari, kwa njia isiyo sahihi katika barabara ya njia moja, kulingana na hati za Mahakama.
Polisi walipekua begi jeusi alilokuwa amevaa wakati huo na inadaiwa walipata sacheti mbili ndogo za bangi.
Kufuatia tukio hilo, Polisi walisema katika taarifa kwamba watu watano waliohusishwa naye pia walikamatwa.
Wakili wa Bw. Mugabe amesema wanapanga kukana mashtaka, na kupinga madai yaliyotolewa na polisi.
Mtoto huyo wa Mugabe aliyekuwa amevaa kofia nyekundu huku akiwa anazungumza na simu yake alipokuwa akiongozwa kwenda katika Mahakama siku ya Alhamisi alizungukwa na watu na hakuwa amefungwa pingu.
Mahakama ilimuweka rumande mtoto huyo wa Mugabe akisubiri uamuzi wa dhamana siku ya Ijumaa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.