#HABARI: Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imeongeza muda wa udahili wa wanafunzi wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026 kupitia Awamu ya Tatu. Udahili huo utaanza tarehe 6 hadi 10 Oktoba mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa Tume huyo Prof. Charles Kihampa amesema Majina ya wanafunzi waliodahiliwa yatatangazwa Oktoba 20 na uthibitisho wa udahili kwa waliopangiwa zaidi ya chuo kimoja utafanyika kuanzia Oktoba 20 hadi Novemba 3.
TCU imewataka waombaji wote kutumia fursa hii ya mwisho kujiunga na elimu ya juu nchini.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.