
NAIROBI – Jiji la Nairobi litakuwa mwenyeji wa tamasha kubwa la kwanza barani Afrika linalolenga kuweka mikakati ya kutoa fidia na haki za kutokana na dhuluma za kihistoria. Tamasha hilo, Ni Wakati Wetu – Kupinga, Kutengeneza na Kudai Upya, litafanyika tarehe 22 na 23 Oktoba 2025 katika kituo cha Entim Sidai.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ni tamasha likalowata pamoja wasanii, wanaharakati, wanamuziki, wataalamu wa sera, wahisani na walimu wa utamaduni kushiriki mijadala ya masuala makuu yanayohusu haki ya kiuchumi na mazingira ukoloni na athari zake kipindi hiki.
Tamasha hili linaendana na azimio la Umoja wa Afrika (AU) ambapo mwezi Februari mwaka huu lilitangaza kuwa mwaka 2025 ni wa Haki kwa Waafrika na watu wenye asili ya Kiafrika, likilenga mjadala wa fidia. AU pia imeweka mikakati ya kufaniksha hatua hiyo kwa kutangaza kuwa kipindi cha mwaka 2026 hadi mwaka 2036 kitatumika kutoa fidia.
Kwa mujibu wa waandaaji, tamasha hili litaunganisha harakati za kijamii na kazi za kifasihi na kisanaa ili kufikisha hoja za fidia nje ya kumbi za mikutano na kuwa mjadala wa kijamii. dkt Liliane Umubyeyi kutoka African Futures Lab alisema changamoto za kisasa kama mabadiliko ya tabianchi, madeni na uhamiaji wa kulazimishwa zinaendeleza mfumo wa kimataifa wa ubaguzi wa rangi.
Washiriki pia wanatarajia kushuhudia midahalo, maonesho ya filamu, muziki, sanaa za jukwaani na tiba za kiafrika kwa ajili ya kutuliza jamii.
Hii ni mara ya kwanza kwa tamasha la aina hii kufanyika barani Afrika na limepangwa kuendelezwa kila baada ya miaka miwili hadi 2035, likilenga kujenga daraja kati ya bara hili na mabara mengine, na kuweka wazi kwamba haki ya fidia si mada ya kisiasa pekee, bali pia ni harakati ya kitamaduni na kijamii.