Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema serikali inaendelea na mikakati ya kuongeza thamani ya zao la zabibu ili wakulima wanufaike zaidi.
Ameeleza kuwa mkoa huo tayari umepata kiwanda cha kuchakata na kuhifadhi zabibu, hatua itakayopunguza changamoto za masoko na kuongeza kipato kwa wakulima.
#AzamTVUpdates
✍Alpha Jenipher
Mhariri | John Mbalamwezi