Akizungumza katika kikao cha majadiliano cha Valdai kilichofanyika mjini Sochi siku ya Alhamisi, Putin ameeleza kuwa hatua hiyo ya Marekani haitakuwa tu msaada wa kijeshi, bali itatafsiriwa kama ushiriki wa moja kwa moja wa kijeshi wa Marekani katika vita vinavyoendelea.

Putin amesisitiza hatari ya hali hiyo, akielezea uwezo wa makombora ya Tomahawk kuidhuru Urusi, na kuongeza kwamba hata iwapo Ukraine itapewa makombora hayo, haitabadilisha chochote katika uwanja wa vita.

Pia ameonya kwamba hatua hiyo inaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa uhusiano kati ya Urusi na Marekani.

Kauli ya Putin ameitoa katika wakati ambapo mataifa ya Magharibi yanatathmini uwezekano wa kuchukua hatua zaidi za kijeshi na kuiwekea vikwazo zaidi Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *