Kulingana na polisi, watu kadhaa waliripoti kuwa wameona droni karibu na uwanja huo. Uongozi wa uwanja wa ndege wa Munich umesema ndege 17 zilishindwa kuanza safari na kuwaathiri karibu wasafiri 3,000. Ndege 15 zilizokuwa zimepangiwa kutua uwanjani hapo zilielekezwa katika viwanja vya ndege vya Stuttgart, Nuremberg, Vienna na Frankfurt.

Ongezeko la kitisho cha droni

Mamlaka ya kudhibiti safari za anga ya Ujerumani imesema kutatizwa kwa shughuli za usafiri kutokana na droni kushuhudiwa katika viwanja vya ndege kote nchini humo kumeongezeka pakubwa. Wiki iliyopita, mamlaka hiyo iliripoti matukio 144 ya kuvurugika kwa safari za ndege kutokana na kitisho cha droni kufikia Agosti mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *