
Mullally mwenye miaka 63 anakuwa pia mkuu wa takriban Wafuasi milioni 85 wa madhehebu ya Anglikana japo hana mamlaka makubwa.
Aziba nafasi ya Justin Welby
Mfalme Charles III ndiye kiongozi wa juu kabisa wa Kanisa hilo la Uingereza nafasi iliyoanzishwa katika karne ya 16 baada ya Mfalme Henry VIII kujitenga na Kanisa Katoliki. Kanisa hilo halikuwa na kiongozi tangu Novemba mwaka uliopita baada ya Justin Welby kujiuzulu kwa kuficha kashfa ya unyanyasaji kwa watoto.