Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita imewataka viongozi wa dini nchini kuweka kipaumbele katika kutoa elimu na mahubiri yenye kukemea rushwa kwa waumini wao.
Hayo yamesemwa na Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, Alex Mpemba na kuongeza kuwa licha ya viongozi hao kuwa na nafasi ya kupandikiza imani pia wanaweza kukemea na kukataza waumini wao kujihusisha na rushwa.
#AzamTvupdates
✍ Ester Sumira
Mhariri |@moseskwindi