Sarah Mullally ameteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Canterbury, mwanamke wa kwanza kuwa katika nafasi hiyo katika historia ya Kanisa la Angilikana duniani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Akiwa na mwenye umri wa miaka 63, anakuwa Askofu Mkuu wa Canterbury, katika Kanisa la Anglikana nchini Uingereza, na kabla ya nafasi hii mpya, alikuwa Askofu wa London tangu mwaka 2018, wakati iliporuhusiwa kuwa wanawake wanaweza kuwa maaskofu kwenye Kanisa hilo.
Nesi huyo wa zamani, anaingia katika vitabu vya historia ya Kanisa hilo, nchini Uingereza ambalo linaendelea kukumbwa na kashfa mbalimbali kuhusu msimamo wake kuhusu ndoa ya jinsia moja na sakata la unyanyasaji wa watoto.

Katiba hotuba yake ya kwanza, ameahidi kulinda umoja wa Kanisa hilo na kuhakikisha kuwa waumini wake wanakuwa salama, na kuongeza kuwa anakabiliwa na kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa Kanisani hilo linakuwa moja.
Baada ya kuteuliwa na Kamati maalum, anatarajiwa kuchukua nafais ya mtangulizi wake, Justin Welby, mapema mwaka ujao, ambaye alijiuzulu mapema mwaka huu, kufuatia kashfa ya Kanisa hilo kutozungumzia ripoti za wavulana kunyanyaswa, miaka ya sabini.

Kanisa Anglikana duniani, lina waumini zaidi ya Milioni 85 katika nchi 165, lakini kila nchi inajitegemea na kujitawala, ila Askofu Mkuu wa Canterbury, anaonekana kiunganisha cha Kanisa Anglikana duniani.