
Wizara ya Ulinzi na ya Mambo ya Kigeni zimesema mifumo ya anga ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Maiquetia ilizibaini ndege za Marekani zikiwa kilometa 75 kutoka Pwani.
Mwezi uliopita Rais Donald Trump alipeleka ndege na Manowari nane nchini Puerto Rico ambayo ni nchi ya Karibiki iliyo chini ya himaya ya Marekani. Hatua hiyo ni sehemu ya operesheni yake ya kukabiliana na dawa za kulevya.
Marekani na mashambulizi ya meli Karibiki
Marekani imezishambulia meli kadhaa za Venezuela katika eneo hilo wiki za hivi karibuni na kuwaua watu 14 wanaodaiwa kuhusika kusafirisha dawa za kulevya kutoka Karibiki kwenda Marekani. Rais wa Venezuela Nicolas Maduro hata hivyo amekanusha madai hayo huku akimtuhumu Trump kuwa anataka kufanya mabadiliko ya kiutawala.